Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii nje ya Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, akithibitisha taarifa iliyokuwa ikizagaa mitandaoni ya Wagombea Urais walioingia katika hatua ya tano bora, ambao aliwataja kuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba pamoja na Balozi Amina Salum Ali. Majina hayo yanapelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kujadiliwa na kupatikana matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu na kupatikana moja ambaye ndie atakuwa Mgombea Urais.

Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa nje ya Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2015

    Wamisionari wawili na wanayala watatu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2015

    Atakayeshinda mwisho wa siku namshauri aimbe na msaniii mahiri waa Tanzania Edson Mwasabwite wimbo wa ni kwa neema tu na rehema, haikuwa rahisi Mungu tu anasaiidia. Atakayeshinda Oktoba aimbe na Kristina Shusho Umenifanya ningare wakati akishukuru Mungu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2015

    Watia nia ambao hawakupita tunawashukuru hatuwezi kuwaacha bila wimbo kwa sababu mmetunogeshea kinyanganyiro. Naona niwape wimbo wa msanii Upendo Nkone ukiniona niko kwenye shida niombee. Mjitie moyo nyie mnaendelea kuwa viongozi pale mlipo na kutimiza ahadi mlizotwambia kunawezekana. Wale walioambatana na wake zao nao walinogesha kampeni tunawashukuru. Cha muhimu ni kuungana kama watanzania, amani ya Tanzania pia ni muhimu ili tuendelee na shughuli zetu za maisha. Tuchague viongozi Oktoba kwa Amani atakayechaguliwa atakuwa mtanzania twende mbele kimaendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...