Waandishi
wa Vyombo mbali mbali vya habari nchini Tanzania na nje walioweka kambi kwenye
Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma kwa ajili ya
kutoa taarifa za vikao mbali mbali vinavyopendelea ili kumpata mgombea
Urais wa Mwaka 2015 kupitia chama hicho.
UPDATES: Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kimemalizika hapa Dodoma na Nape Nnauye akiongea na wanahabari hivi punde amesema kikao kimaeenda vyema kabisa na kumalizika vizuri - ila majina hatoyataja sasa. Hadi kesho saa nne asubuhi....
UPDATES: Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kimemalizika hapa Dodoma na Nape Nnauye akiongea na wanahabari hivi punde amesema kikao kimaeenda vyema kabisa na kumalizika vizuri - ila majina hatoyataja sasa. Hadi kesho saa nne asubuhi....
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(wa pili kushoto) akiongoza kikao cha Kamati Kuu Maalum cha CCM mjini Dodoma, Kikao hicho kitachuja majina ya wagombea na kupata majina matano(5) .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa taarifa fupi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Kamati Kuu Maalum ambapo wajumbe 28 walihudhuria kati ya 32.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakipitia baadhi ya makabrasha wakati wa kikao cha Kamati Kuu Maalum (Picha na Adam Mzee)
Vijana wa CCM wakipakia mikoba yenye makabrasha ya mkutano maalum wa CCM Taifa 2015 unaotarajiwa kuanza baadaye leo katika ukumbi mpya wa Dodoma Convention Centre mjini Dodoma uliozinduliwa juzi.
Hello Michuzi tunakutegemea sana hasa mashariki ya mbali.....Chennai India. Tupo huku kwa libeneke la raha zetu. Endelea bila wasi kutupa breaking news za matokeo ya CCM hapo Dom.
ReplyDeleteMbona updates hazibadiliki Michuzi? Tujuze nini kinaendelea mkuu.tunakutegemea
ReplyDeleteNi lowasa Tu ndio anapita
ReplyDeleteKazi nzuri Michuzi, kinachotia raha Ni uwezo wako wa kutoa taarifa sahihi. Hongera Sana naana Ni wazi mchakato wa CCM kwa 99% ndiyo unamtoa Rais!!
ReplyDeleteTuwe Waungwana....Michuzi anatoa anachopewa.....apike data!!!! Tutulie.
ReplyDeleteJagular umebebeshwa LUMBESA?? Muogopeni Maulana jamani eh!
ReplyDeleteNi Magufuli ndio atateuliwa.
ReplyDeleteNi Magufli ndio atakaepita.
ReplyDeleteNaungana na huyo anaekisia kuwa Magufuli ndiye atakayepita kwa sababu Magufuli ni mchapakazi na hana mzaha na mtu. Kama vile vile kila Wizara aliyopewa alifanya vizuri sana basi hata akifaulu kuwa Rais wa nchi yetu most likely ni kwamba wembe wake utakuwa ni ule ule na hata kupita.
ReplyDeleteMagufuli hafai ubabe mwingi sana tunataka kiongozi mpole na mstaarabu kama lowasa au bilal
ReplyDeletehello michuzi
ReplyDeletepole kwa majukumu
Hapa mambo hayaendi kazi haifanyiki wapeznzi wa siasa tunataka upadates toka dodoma yaani toka majira ya saa mbili tupo online kuona lolote ila kimya atleast tumepata update saa sita tafadhali tunaomba update angalao tuendelee na kazi za mwekezaji!!!!duuuu
kazi hazifanyiki huku asubuhi mbali kiu ya kujua ndo imepanda saaana
Majina ni lowasa, Asha migiro,Bilal, Membe na Magufuli. Na kinyangiro ni Kati ya Lowasa na Asha Migiro.
ReplyDeleteMajina yanatolewa leo saa nne ya asubui
ReplyDeleteSo stay tunned na pia yatarushwa moja kwa moja kwenye radio
Majina yanatajwa kesho asubui
ReplyDeleteMajina yaliyppitishwa ni:
ReplyDelete1. Bernad Membe
2.John Pombe Magufuli
3. Asha Rose Migiro
4. January Makamba
5.Amina Ali Salum
Ccm tangazeni majina munaogopa nini? Mara hii ndio kifo chenu mukichemsha kuweka mgombea mzuri mumekwisha
ReplyDelete