Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umesema kuwa mgombea wao wa Urais watamtoa baada ya siku saba.

Akizungumza na Waandishi wa Habari usiku huu,Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, Mhe. James Mbatia amesema kuwa kuchukua muda mrefu kwa kikao hicho imetokana na kuandaa utaratibu jinsi ya kumtoa mwali wao  wa Urais kwa tiketi ya UKAWA aliye bora. Amesema kuwa mkutano huo pia umechukua muda mrefu  kutokana na mambo mengi ikiwemo mgawanyo wa majimbo.

Afisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Tumaini Makene akizungumza na waandishi habari  hivi punde juu kinachoendelea katika mkutano wa kutafuta mgombea wa Urais kwa tiketi ya UKAWA, uliofanyika katika Hoteli ya Colesseum jijini Dar es Salaam,Makene amesema majadiliano hayo sio urais tu bali kuna mipaka ya majimbo mapya jinsi watavyojipanga katika kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. Makene amezidi kuwataka waandishi wawe na subira kusubiri maamuzi yatakayotoka katika kikao hicho ambacho kimeanza tangu asubuhi ya leo. 
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu mchana,Waandishi wa Habari waliopiga kambi wakisubiri kupata jina la mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam,wakajikuta wanaacha stendi za Camera zao na kukaa pembeni wakisubiri lolote litakalojiri.
Waandishi wa Habari wakiwa wameweka kambi tangu saa saba mchana wakisubiri kupata jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam, hiyo inatokana na taarifa zilizotolewa na UKAWA kuwa leo ndio siku rasmi ya kutangaza jina hilo lakini masaa yanazidi kwenda huku kikao chao kikiwa kinaendelea.
Waandishi wakisubiri mtu wa kutoa taarifa juu ya jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, ambapo taarifa hizo za kuja mtu huyo ziligonga mwamba na kuambiwa kilichobaki ni makubaliano suala jinsi kuendesha uchaguzi katika majimbo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hapo kutakua na tatizo maana walisema ndani ya saa 24 tutatangaziwa sasa imekua siku saba. Hapo bwana kila mtu anataka lipumba hakubali na slaa halikazalika sasa patamu hapo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2015

    Ukawa mmekwama.Maji na Mafuta huwa havichanganyiki

    ReplyDelete
  3. Ukawa wamechemsha sana, hakuna upinzani Tanzania hao viongozi wa ukawa wote ni waganga njaa tuu na hilo ndo tatizo kubwa.Hawataki kuwaachia na wengine wagombee urais wamehodhi madaraka na tena kidictator!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2015

    Hahahahahaha, Hapo ndipo tunaamini sasa kuwa CCM imezingatia temokrasia ya kweli, mfano watangaza nia wangekuwa wengi kama wa CCM ingekuwaje, si ingewachukuwa mwaka mzima kufanya maamuzi. CCM inataendelea kushinda tu maana kila uchaguzi wanakuja na sura mpya huku kwetu wazee wale wale wanang'ang'ania, wangemsikiliza ZOTTO wangeelewa somo.

    Mimi nipo UKAWA lakini nimejifunza kitu kupitia CCM, ntampigia wa CCM tu, huku kwetu hakuna jipya, vinana tumewabeba sana, lakini wazee wanatuangusha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 15, 2015

    ati hawa ndo wanataka kuleta mabadiliko wakati wenyewe wanahitaji mabadiliko kwenye oblangata zao kwanza , ni waroho na walafi wa madaraka hata wao wakipewa nchi wataiba vile vile wameonyesha upuuzi wao mapema mnoo.
    magufuli atawatoa jasho kwenye meno hata mkimtoa mwali wenu mwezi ujao ikulu mtaiona kwa macho hadi mjifunze siasa bora na sio matumbo yenu. yaani mna tamaa mno mnajidai kuwaponda ccm wakati nyie hamfai ina maana muda woote mlikuwa hamjui mtamsimamisha nani? ni aibu kubwa sana yani hata watia nia hakuna manake mabosi wenu wanawaita wasaliti ilihali wao waendelee kuwakalia kimabavu madikteta wakubwa. siipendi ccm lakini mimi na familia yangu kura tutampa Magufuli yes magufuli ni mchapa kazi hataree na sio nyie bla bla kibao nyani haoni kundule. ni hayo tuu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...