Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katika hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana  jijini Johannesburg mbali na mambo mengine nilihimiza sana ushirikiano baina yetu kwani wahalifu mtandao wameendelea kua mbele yetu kutokana na ushirikiano mkubwa waliokua nao. Ushirikiano unao mabatana na kusambaza vitendea uhalifu mtandao bure auu kwa gharama nafuu mitandaoni.

Baada ya kulizungumza hili laushirikiano wazungumzaji wengine wote walionekana kuniunga mkono na hatimae kuonekana ni swala muhimu lakufanyiwa kazi mapema. Nafarijika kuona Uingereza tayari mukuu wake wa CERT ametilia mkazo kauli hii (Ya ushirikiano) kupitia kikao kilicho malizika London ambapo taarifa kamili kuhusiana na hili inaweza kusomeka kwa “KUBOFYA HAPA

Aidha, Marekani na Israel baada ya kutia saini makubaliano ya kuboresha ushirikiano katika maswala ya usalama mitandao paliambatana na kuhimiza mataifa mengine kuona umuhimu wa kushirikiana katika vita hii ya uhalifu mtandao.
Nilipata kuzungumza tena katika mkutano wa wanausalama Nchini Cyprus ambapo pia nilizungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na ushirikiano huku nikipongeza umoja wa ulaya kwa kuungana kwao katika hili la usalama mitandao kupitia chombo chao kiitwacho ENISA kinacho hudumia mataifa yote yaliyo ndani muungano wa nchi za ulaya katika maswala ya Usalama mitandao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...