SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO),  LINAWATANGAZIA  WAKAZI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM NA MJI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI  KUWA, UTARATIBU WA KUPATA BILI KWA MTEJA UMEBADILIKA KUTOKA “SPOT BILL” KWENDA “SPOT SMS” KUANZIA  JULAI 2015.

UTARATIBU HUU UNAMAANISHA KUWA MTEJA ATAKUWA AKIPATIWA BILL YAKE YA MATUMIZI YA MAJI KILA MWEZI KUPITIA SIMU YAKE YA MKONONI, NA UTALENGA WATEJA WA MAJUMBANI TU NA HAUTAHUSISHA KAMPUNI NA TAASISI ZA SERIKALI.

FAIDA ZA UTARATIBU HUU NI PAMOJA NA :
1. KUBORESHA HUDUMA KWA MTEJA NA KUONGEZA MAWASILIANO YA MOJA KWA MOJA KATI YA SHIRIKA NA MTEJA
2. MAENDELEO YA TECKNOLOJIA YANAKOPELEKEA UMUHIMU WA HUDUMA HII
3. KUONGEZA WIGO WA ULIPAJI KWA MTEJA
4. KUPUNGUZA GHARAMA ZA UTARATIBU WA AWALI

NAMNA MTEJA ANAWEZA KUJISAJILI KUPATA HUDUMA HII KUPITIA NJIA ZIFUATAZO

1. TOVUTI YA SHIRIKA www.dawasco.com
2. KUMPA MSOMA MITA WA DAWASCO TAARIFA ZAKO
3. KUFIKA OFISI YOYOTE YA DAWASCO ILIYO KARIBU NAWE

EWE MTEJA, TOA NAMBA YAKO YA SIMU ILIYO SAHIHI ILI KUPATA BILI YAKO KILA MWEZI NA KUEPUKA USUMBUFU WA KUKATIWA HUDUMA HII .
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022- 2194800 AU 0658-198889       

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO MBELE KWA MBELE”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...