JOTO la Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, limepanda kwa kila rika la wazee, vijana , na akina mama, ambapo kila mmoja amekuwa anatazama Jimbo la kugombea kupitia chama anachokiamini katika ngazi ya Udiwani na Ubunge. Walter Nnko ni Daktari mzalendo na kamanda wa vijana kondo/kunduchi.

 Dr. Walter Nnko amechukuwa fomu ya ubunge jimbo la kawe na muda ukifika atawaomba wanachama wa CCM wampe ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi wa kumi MWAKA huu. 

Anaamini kuwa amesheheni majawabu ya kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kawe. Akizungumza nasi Jumatano amesema, ni wakati wa vijana wasomi kuonyesha elimu zao kwa vitendo, na kurejesha faida ya fedha za umma zilizowasomesha wakiwa vyuoni kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo. "Nataka nilipe fadhila za wananchi wa Jimbo la KAWE kwa kuwatumikia kuyafikia maendeleo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)" amesema Dk.Nnko.

 Anabainisha kuwa kiu yake ni kuhakikisha wananchi wa Jimbo la KAWE wanapata huduma nzuri za afya, elimu bora, ajira na bila kusahau miundo mbinu. "Naheshimu kampeni ya Mwenyekiti wa taifa wa chama chetu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuamsha ari ya kuboresha elimu ya sekondari kwa kuhakikisha maabara zinajengwa" anasema Nnko. 

Anasema endapo atapata nafasi hiyo ya kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo ilo atahakikisha anafanya mbinu zote kuongeza shule za kata, zahanati kwenye kila kata, atasimamia ujenzi unaoendelea wa Hospitali ya rufaa inayojengwa mji mpya, kata ya Mabwepande ili kuhakikisha jimbo la Kawe lina huduma nzuri za afya, kupata vifaa vya maabara na kujenga maabara za kutosha, anadai kuwa majengo bila vifaa yanapoteza maana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...