Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ,Jasper Mero akizungumza katika mkutano wa Wadau wa Kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa ofisi ya CAG uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ,Jasper Mero (mwenye tai katikat)akiwa katika picha ya pamoja na wadau kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa ofisi ya CAG uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jami.
Imeelezwa kuwa kufikia mlaengo kwa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) inategemea na mchango wa wadau mbalimbali katika kupanga
mikakati ya kuweza ofisi ya CAG kusimamia pamoja na kutekeleza.
Hayo ameyasema leo,Kaimu Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Jasper Mero wakati akifungua mkutano
wa wadau wa kuandaa mikakati ya Ofisi
ya CAG ya 2016 -2021 katika kuweza ofisi hiyto iweze kusimamia mikakati
hiyo.
Amesema wadau wametakiwa kutoa maoni
kwa uhuru katika ofisi hiyo iweze kupata mikakati ya kuweza kusimamia katika
udhibiti wa fedha ya Umma.
Mero amesema mikakati ya 2011hadi
2016 imetekekelezwa kwa asilimia 100 hiyo ikiwa imetokana na mahusiano ya ofisi
ya CAG pamoja na wadau ambao walitoa maoni chanya katika ofisi hiyo.
Amesema katika ofisi ya CAG imepata
mafanikio ikiwa ni pamoja kutoa ripoti za mara kwa mara pamoja na kutoa ushauri
wa kiutekelezaji kutokana na ukaguzi walioufanya katika mashirika ya Umma
,pamoja na Taasisi za Serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...