Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto) akimkabidhi Fatuma Khamis mkazi wa Kwamtogole – Tandale jijini Dar es Salaam (wa tatu toka kushoto) mfuko wa maharage ikiwa ni moja kati ya vyakula mbalimbali alivyokabidhiwa ikiwa ni msaada ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa ushirikiano na Doris Foundation. Wanaoshuhudia Grace Lyon (kulia) na Doris Mollel (wa pili toka kushoto).
Baadhi ya wakazi wa Kwamtogole – Tandale jijini Dar es salaam wakiwa wanasubiria kugawiwa vyakula mbalimbali vikiwa kwenye vikapu maalum vilivyotolewa msaada na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa ushirikiano na Doris Mollel Foundation kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kushoto) akiongozana na baadhi ya washirika wenza kutoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa baadhi ya wakazi wa Kwamtogole –Tandale jijini Dar es Salaam kwa ajilli ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa ushirikiano na Doris Mollel Foundation.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania pamoja na Doris Mollel Foundation wakiwa wamebeba vikapu vyenye vyakula mbalimbali kwa ajili ya kutoa msaada kwa wakazi wa Kwamtogole – Tandale jijini Dar es Salaam. Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa kushirikiana na Doris Mollel Foundation kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mkazi wa Kwamtogole –Tandale jijini Dar es Salaam Bi.Taabu Abdallah (kushoto) akikabidhiwa msaada wa vyakula mbalimbali na Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza. Msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom kwa ushirikiano wa Doris Mollel Foundation kwa ajilli ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...