Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WANANCHI wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika zoezi la kujiandikisha
katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa mfumo wa BVR lililoanza leo.
Wakizungumza na Globu ya Jamii kwa
nyakati tofauti walisema zoezi linaenda vizuri lakini linakabiliwa na
changamoto chache ambazo zikitatuliwa wananchi wote watajiandikisha katika
Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.
Akizungumzia suala kujiandikisha
katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ,Salumu Abbakari Mkazi wa Msisiri
amesema kuwa alifika mapema na kuweza kujiandikisha lakini ameona kuna
changamoto ya kituo kuzidiwa na watu.
Aidha amesema watu wasikilize maneno
ya mtaani juu ya changamoto za kujiandikisha wafike na kuweza kujiandikisha
wasikate tama wakati hawajafika eneo la tukio.
Abbakari amesema NEC wamejipanga
vizuri kuandaa utaratibu lakini changamoto hazikwepeki baadhi ya kulalamika
kutokana na kutokuwa wavumilivu wakiwemo vijana.
Nae Sophia Thomas amesema kuwa idadi
ya waandikishaji iongezeke katika kuweza kuondoa changamoto ya wananchi kukaa kwa muda
mrefu.
Amesema changmoto zilizopo katika
kituo haziwezi zikamfanya asijiandikishe kwani kura yake ni muhimu hivyo
atajiandikisha na kuweza kupiga kura.
Wananchi wa Kata ya Mwananyamala
wakiwa katika foleni kujiandikisha
katika Daftari la Kudumu Mpiga Kura katika mfumo wa alama za vidole (BVR), leo
jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akiwa amekaa kwenye kiti
kwa ajili ya kupiga picha ya kitambulisho cha kupigia kura katika zoezi
kuandikisha wananchi Daftari la Wapiga kura kwa mfumo wa alama ya Vidole BVR
katika Kituo cha Kujiandikishia cha Shule ya msingi Kambangwa Wialya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...