Na John Nditi, Morogoro
MKUU wa Mkoa wa Morogoro pichani kati, Dk Rajab Rutengwe, amewaomba wanawake kuanzia ngazi ya mitaa, vitongoji, vijiji na kata kushiriki katika suala la ulinzi shirikishi kwa kuwafichua wahalifu wanaotishia kuhatarisha uvujifu wa amani ndani ya mkoa.
Dk Rutengwe alitoa rai hiyo wakati alipozungumza na wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Morogoro , Julai 24, 2015 wilayani Kilosa baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa viti maalumu kwa makundi matano , UWT Mkoa, watu wenye ulemavu, Taasisi za Vyuo Vikuu, Wafanyakazi, NGO’s.
Hivyo aliwaomba wanawake kuunga mkono juhudi za serikali ya kukabiliana na uharifu wowote kushiriki katika ulinzi shirikishi kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kwa watu wanaoshuku kuwa na mienendo isiyofahamika maeneo wanakoishi.
Pia aliomba kamati ya ulinzi na usalama mitaa, vitongoji , vijiji na kata ziwajibike katika majukumu ya kufanya kazi zao za kubaini waharifu.
Mbali na hayo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa madhehabu mbalimbali ndani ya mkoa kuwafichua watu wanaogeuza nyumba za ibada kuwa ni sehemu ya maficho yao ya kupanga ama kutekeleza vitendo vya kiharifu hali inayoweza kutoa taswira potovu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...