Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na viongozi wa wizara
mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya kuzindua kikosi kazi cha
kupambana na uhalifu wa kimazingira nchini
kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu
pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa
kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii,
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu akizungumza na viongozi wa wizara
mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto-meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha
kupambana na uhalifu wa kimazingira
nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti
haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Katika hotuba yake IGP Mangu
aliomba ushirikiano na wananchi katika kupambana na uharibifu wa mazingira nchini. Tukio la uzinduzi huo
lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
Makamu
Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Utunzaji wa Mazingira (ICCF) la nchini
Marekani, Dk Kaush Arha akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali nchini pamoja
na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (kulia meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha kupambana na uhalifu
wa kimazingira kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa
miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu nchini. Uuzinduzi huo ulifanyika
katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini (IGP), Ernest Mangu
Viongozi
mbalimbali wa Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi pamoja na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa
akizindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini
kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu
pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika
Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa
habari mara baada ya kuzindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa
kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji
wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho
kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili
na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini
Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...