Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kakukuru,Ukerewe ikiwa siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Mwanza.
Katibu Mkuu amekamilisha ziara ya kutembelea majimbo yote ya Uchaguzi nchi nzima ambapo amejionea utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi unavyooendelea pamoja na uhai wa Chama Cha Mapinduzi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo akihutubia wakazi wa Kakukuru wilayani Ukerewe.
Wakazi wa Kakukuru ,Ukerewe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuzindua shina la wakereketwa wa CCM Kakukuru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya maendeleo ya mradi wa maji Kazilankanda uliopo kijiji cha Chabilungo ,Ukerewe utakaonufaisha vijiji 13 kutoka kwa msimamizi wa mradi Revocatus Migarambo .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Nansio katika Uwanja cha Mongella ambapo aliwaambia wananchi hao wasichagueviongozi kishabiki kwani ushabiki unaweza wachelewesha sana kimaendeleo,alitoa mfano halmashauri ya wilaya ya Ukerewe ipo upinzani na hakuna jambo la maendeleo linafanyika mpaka sasa.
Ukerewe jamani, hata jukwaa la kusimamia badala ya hicho kiti?
ReplyDelete