Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Lawrence Masha Akifurahia Jambo na Wakili  Peter kibatala
(wa kwanza kulia)   na Albart Msando (wa pili kushoto)
 Masha aliyevaa tisheti jeusi suruali ya jinsi ya rangi ya Bluu akifurahia jambo  na mawakili na marafiki zake  muda mfupi baada ya kupata dhamana
--
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Lawrence Masha (45) baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Masha alifikishwa mahakamani hapo jana nyakati za saa 6:49 mchana na kuhifadhiwa mahabusu na ilipofika saa 9:31 alasiri alipelekwa mbele ya Hakimu Mkazi  Mkuu, Waliarwande Lema kwa ajili ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Masha aliachiwa huru baada ya nyaraka za wadhamini wake wawili wanaoaminika ambao kila mmoja alisaini bondi ya Sh 1milioni kuhakikiwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuithibitishia mahakama kuwa nyalaka hizo ni halali.
Kufanyika kwa uthibisho huo wa nyaraka za wadhamini ndio uliopelekea juzi Masha kupelekwa mahabusu katika gereza la Segerea.
Baada ya kumaliza kukamilisha taratibu hizo za dhamana ilipofika saa 9:46 alasiri Masha, mkewe, mawakili wanaomtetea katika kesi hiyo, Peter kibatala na Albart Msando pamoja na ndugu zao wengine waliondoka mahakamani hapo kwenda nyumbani.
Awali Agosti 25, 2015 Masha alipandishwa kizimbani akikabiliwa na shtaka la kutumia lugha ya matusi kwa maofisa wa Jeshi la Polisi.
Masha aliyekuwa amevaa tisheti jeusi, suruali ya jinsi ya rangi ya Bluu na viatu aina Sendo anadaiwa kuwa Agosti 24,2015  katika kituo cha polisi cha Osterbay alitoa lugha ya matusi kwa maofisa wa jeshi la polisi.
Chanzo: Mwananchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...