Wajasiriamali nchini wamehamasishwa kujiunga na vikundi vya VICOBA nchini ili waweze kujipatia maendeleo kwa haraka.
Inasemekana kwamba kujiunga na vikundi hivyo, kutasaidia wananchi kujipatia faida mbalimbali kama kujifunza utamaduni wa kuweka akiba kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa wakati wa uzinduzi wa kadi maalum ya Benki ya Posta (ATM card) kwa ajili ya vikundi vya VICOBA nchini.
Kadi hiyo iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam inatazamiwa kuwarahisishia wanachama wa VICOBA pale wanapokuwa wakishughulikia maswala ya kibenki.
Juhudi za kuja na wazo hilo ni matunda ya pamoja ya Benki ya Posta Tanzania, Taasisi ya Maendeleo Endelevu ya VICOBA na NEEC.
Kwa sasa, mtandao wa VICOBA una vikundi zaidi ya 5,000 katika mikoa 30.
“Hii ni hatua muhimu sana,” alisema Bi. Beng’i.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta, Prof. Leticia Rutashobya alisema uzinduzi wa kadi hiyo maalum ya ATM ni ushahidi tosha kuwa benki hiyo imedhamiria kusaidia wajasiriamali hapa nchini.
“Tuna fuhara kusaidia na kufanya kazi na wajasiriamali katika nchi yetu,” alisema.
Naye Mratibu wa maswala ya afya katika taasisi hiyo ya VICOBA, Bi. Ikupa Njela alisema kadi hiyo ni ushindi kwa wanachama wa VICOBA pote nchini.
“Kadi hii itasaidia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya vikundi hivi katika nchi yetu,” alisema.
Hivi karibuni, NEEC ilitangaza kutoa shilingi milioni 700 kwa Benki ya Posta Tanzania kama dhamana ya mikopo itakayotolewa na benki hiyo kwa wajasiriamali hapa nchni.
Mpango huu uko chini ya Mfuko wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ulioanzishwa mwaka 2008 ambao pamoja na majukumu mengine unatumika kutoa au kudhamini mikopo yenye masharti nafuu kwa wajasiriamali nchini.
Fedha hizo zitawekwa katika akaunti maalum katika Benki ya Posta kama dhamana ya mikopo na benki hiyo itatumia fedha zake kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa makundi husika kwa kiwango cha mara tatu ya dhamana iliyowekwa na Baraza.
Mikopo itatolewa kwa riba ya asilimia 11 kwa mwaka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta, Profesa Leticia
Rutashobya (katikati) akiwa mwenye furaha wakati wa uzinduzi wa kadi maalum ya
ATM ya benki hiyo kwa ajili ya vikundi vya VICOBA hapa nchini iliyozinduliwa
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Wengine katika picha ni Katibu Mtendaji wa Bazara la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (kushoto) na Rais wa
VICOBA, Bi. Devota Likokola.
Sehemu ya wanachama wa VICOBA nchini wakifuatilia
uzinduzi wa kadi maalum ya ATM ya Benki ya Posta kwa ajili ya vikundi vya
VICOBA hapa nchini iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo inatazamiwa kurahisisha utendaji
kazi wa vikundi hivyo katika maswala ya kibenki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta, Profesa Leticia
Rutashobya (kulia) akiwa mwenye furaha wakati wa uzinduzi wa kadi maalum ya ATM
ya benki hiyo kwa ajili ya vikundi vya VICOBA hapa nchini iliyozinduliwa mwishoni
mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Katibu
Mtendaji wa Bazara la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i
Issa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...