Meneja bidhaa wa Benki ya Barclays,Valence Lutegavya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi ya ATM ya dola za kimarekani katika mkutano wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi
wa Benki ya Barclays hapa nchini, Bwana Kumaran Pather.
Meneja bidhaa wa Benki ya Barclays,Valence Lutegavya akionyesha kadi ya ATM ya Dola za Kimarekani katikati ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi
wa Benki ya Barclays Tanzania, Bwana Kumaran Pather na wamwisho ni
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi
wa Benki ya Barclays hapa nchini, Bwana Kumaran Pather, akitoa msisitizo juu ya faida za ATM kadi ya dola za kimarekani kwa wateja watakao zitumia kazi hizo wakati wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali haoa nchini na kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi
wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi
wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar akifafanua juu ya matumizi ya ATM kadi za dola za kimarekani katika matumizi ya kawaida katika kununua bidhaa mbalimbali kwenye maduka yanayotumia kadi za ATM hapa nchini, katika mkutano wa uzinduzi kadi ya ATM ya dola, uliofanyika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam leo.
BENKI ya Barclays hapa nchini imezindua kadi ya ATM ya dola hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi
wa Benki ya Barclays Tanzania, Bwana Kumaran Pather wakati akizungumza
wakati wa uzinduzi, uliofanyika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam leo.
alisema “wateja wa Barclays
wenye akaunti ya Dola za kimarekani wataweza kutumia kadi hizo mpya wakiwa ndani
na nje ya Tanzania kupitia huduma za VISA.”
Kadi
hizi mpya zimewekwa kwenye mfumo mpya wa teknohama ambao unawapa wateja usalama
zaidi wanapofanya huduma zote za kibenki. Mteja atapata fedha za ndani
atakapoitumia kadi hiyo akiwa nchini. Miamala yote ya nje ya nchi itafanyika
kwa dola za Kimarekani tu.
Pia amezitaja faida
za Kadi za dola kutoka Benki ya Barclays hapa nchini, Inarahisisha malipo ya bidhaa na huduma
madukani, hotelini, vituo vya mafuta n.k. nchini na dunia nzima, Utakupo toa hela nje ya nchi kupitia ATM
utapata noti za dola za kimarekani,
Inakupa amani ya akili baada ya kukamilisha
muamala kwa mtandao na pia inakupa nafasi ya kupata punguzo la bei
mtandaoni unapotumia kadi ya matumizi ya Barclays.
Aliendelea kusema “Barclays
inawasaidia wateja kunufaika kwa kulenga kuwapatia uzoefu rahisi na kuwasikiliza
mahitaji yao.” Barclays inazingatia kila wakati kuwapa wateja wake huduma
timilifu za hali ya juu na kwa uzoefu wa hali ya juu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...