CCM Number One ni blogu maalumu iliyoanzishwa kwa ajili ya kuripoti habari zinazohusu mikutano ya kampeni ya mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan wanayoifanya katika mikoa mbalimbali nchini.
Lengo la blogu hii ni kuwafahamisha Watanzania na watu wengine duniani wanaofuatilia uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, nini ambacho wagombea hao wanakizungumza na kuwaahidi Watanzania kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.
Pia imesheheni picha lukuki za wagombea hao wakiwa kwenye mikutano mbalimbali. Lengo ni kuwapa picha halisi Watanzania juu ya kile kinachotokea kwenye mikutano hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...