BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mradi wake wa kuwajengea Uwezo Wabunge na Watumishi (LSP) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kwa mara ya Pili mwaka huu limeratibu Bunge la Vijana kwa kushirikisha Wanafunzi zaidi ya 100 kutoka Taasisi za Elimu ya Juu hapa Nchi ambao ni viongozi katika Serikali zao. Bunge hilo ambalo limeanza Jumamosi tarehe 15 Julai, 2015 na linatarajiwa kumalizika tarehe 19 Julai 2015.
Spika wa Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Baraka Thomas (UDSM) akiongoza vikao vya Bunge
Waziri Mkuu katika Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Alexandra Wasonga (ARDHI) akijibu Maswali ya papo kwa papo Bunge wakati wa Kipindi cha Masuali kwa Waziri Mkuu.
Mwanasheria Mkuu katika Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Gama Zulu Leonidas (SAUT) akiwasilisha Muswada wa Serikali wa Kuanzisha sheria ya Baraza la Vijana la Taifa wa Mwaka 2015 Bungeni jana.
Wajumbe wa Bunge la Vijana wakishiriki Vikao vya Bunge hilo Mjini Dodoma.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...