Hatimaye Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia Programu yake ya Grow ambapo kauli mbiu ni Wekeza kwa wakulima wanawake wadogo wadogo inalipa lafika tamati ambapo kulikuwa na mchuano mkali kati ya washiriki 15 ambao walikuwa katika Kijiji cha Kisanga Wilayani Kisalawe Mkoani Pwani wakiwa na shughuli mbalimbali za Kilimo ambazo zililenga hasa katika kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wanawake. Washiriki hao walikaa kijijini kwa muda wa siku 21 hatimaye kufikia kumpata mshiriki mmoja ambaye amejishindia kiasi cha Tsh 20,000,000 fedha ambazo zitanunua pembejeo za Kilimo. Fainali hizo zilifanyika katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam 
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne akitoa neno la Shukurani kwa ushindi alioupata , Ameshukuru shirika la Oxfam kwa kuendesha shindano hilo na kuahidi kuwa atakwenda kuwa Balozi mzuri na kusema kuwa washiriki wote ni washindi na yeye amepata zawadi hiyo kuwawakilisha wote.

Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa Nne 2015 Bi. Carolina Chilele(Kulia) akikabidhiwa Ngao yake ya Ushindi na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...