
Hatua hiyo Imetokea baada ya wagombea wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Na aliekuwa Mgombea wa Chama cha Wananchi CUF Kutojitokeza Kurudisha Fomu zao hadi Muda Uliopangwa na Tume ya Uchaguzi Kumalizika. Wagombea hao ambao walichukua Fomu na Kutorejesha ni Severin Simon Magwaya (CHADEMA) na Twahil Saidi Namwaga wa CUF.
Jimbo la Nanyamba katika Halmashauri ya Wilaya Ya Mtwara ni Jimbo Jipya Baada ya Kugawanywa Jimbo la Mtwara Vijijini Abdallah Dadi Chikota Ambae Hivi karibuni Aliagana na Wasaidizi wake wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Licha kuanza Harakati zake Za Kisiasa Aliwaomba Kutekeleza Vema Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Mkoa wa Lindi.
Chikota akibainisha Baadhi ya Miradi Hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Wodi ya Kisasa pamoja Nyumba ya Ghorofa itakayokaliwa na Familia 10 za Waganga katika Hospital Ya Sokoine Lindi,Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa
Kufuatia Kutotokea kwa Wagombea hao hii Leo Sasa Inasubiriwa Taratibu za Tume ya Uchaguzi Kumtangaza Rasmi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mkoani Mtwara
Hili suala la 'kupita bila kupingwa' ni upuuzi.
ReplyDeleteHata wakati wa chama kimoja mtu alikuwa anapambanishwa na kivuli. Kwa nini leo hii asipambanishwe na kivuli ili ifahamike kama anakubalika?