Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idris Kikula akimkabidhi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi nakala ya kitambu kinachoelezea kwa kina historia ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Katika Maelezo yake, Prof. Kikula amesema UDOM imeamua kuweka katika maandishi historia nzima ya Chuo hili ili kuepusha upotoshaji na upindishaji wa ukweli na kwamba UDOM inapanga kumuenzi Mhe. Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuanzishwa na hatimaye ujenzi wa UDOM. wengine katika picha kutoka kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo Prof. Shaaban Mlacha anayesimamia masuala ya mipango, fedha na utawala, Naibu Mwakilishi wa Kudumu Balozi Ramadhan Mwinyi na Bi. Christina Silvester, Katibu wa Baraza.
Makamu Mkuu wa UDOM Prof. Kikula akimkabidhi nakala ya kitambu cha historia ya UDOM, Prof. Estomih Mtui, M.D anayefanya kazi Weill Cornel Medical Collage, Prof. Mtui ni moja kati ya wana-Diaspora ambaye amekuwa kiungo kikubwa katika utafutaji na upatikanaji wa vifaa tiba ,vitabu na wataalam wa fani mbalimbali kwaajili ya kusaidia nchini Tanzania. baadhi ya vifaa na vitabu ambavyo Ujumbe wa Makamu Mkuu wa UDOM wamevikagua vimepatikana kwa juhudi za Prof. Mtui
Na Mwandishi Maalum, New York
Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM), kinatarajia kufanya hafla ya aina yake ya kumuenzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kama sehemu ya kutambua mchango wake wa hali na mali uliopelekea kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho cha aina yake
Tanzania na nje ya Tanzania.
Taarifa ya kusudio la Chuo hicho kumuenzi Mh. Rais Kikwete imetolewa mwishoni mwa wiki na Makamu Mkuu wa UDOM, Prof. Idris Kikula wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi na Maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa.Profesa Kikula na ujumbe wake yuko katika ziara ya kikazi nchini Marekani, ziara iliyomfikisha Jijini New York, ambapo ujumbe ulipata fursa ya kukagua vifaa tiba na vitabu vya kiada na ziada ambavyo vimetolewa na wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...