Daktari wa Kwanza Bingwa Mshauri wa Maradhi ya Moyo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro nchini Tanzania Dr.Harun Elmada Nyagori azawadiwa Tuzo ya Kimataifa na kutambuliwa na Baraza la Madaktari Bingwa wa shirikisho la Nchi za Ulaya(European Society of Cardiology) -London Uingereza'
Akipewa hiyo Tuzo ya Heshima na Rais wa Shirikisho Hilo Prof.Pinto alimwelezea imekuwa Historia kubwa kumpata Daktari aliyewakilisha Mada za Utafiti wa Maradhi ya Moyo kutoka Tanzania na hawajawahi kumpata Mtanzania aliyewahi kuingia kwenye Shirikisho Hilo
Hivyo Dr Nyagori amefungua mlango kwa Madaktari wengine kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu hiyo taaluma ya magonjwa ya Moyo.
Dr Nyagori akiwa na muasisi wa Kimataifa na Mwandishi wa Vitabu vikuu wa taaluma hiyo Prof.Eugine Brawnward
Dr Nyagori na Rais wa Shirikisho Hilo la Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Moyo prof.Pinto Dr Nyagori amealikwa na Shirika la Utangazaji BBC kwa mdahalo maalumu kuhusu hiyo Tuzo,taarifa kamili zitarushwa Focus on Africa
Dr Nyagori akiwa na wajumbe wenza walioteuliwa kuingia kwenye Shirikisho Hilo la Madaktari Bingwa wa Ulaya wakiwa na Rais wa Shirikisho Hilo Prof.Pinto
Hongera sana.
ReplyDeleteHongera nyingi sana kwako daktari kwa kupata heshima hiyo iliyotukuka katika masuala ya utafiti wa maradhi ya Moyo yanayoikabili Tanzania.
ReplyDeleteMdau
Christos Papachristou
Diaspora
Not many of these in Bongoland. How on earth is he based in Morogoro and not at Muhimbili?
ReplyDeleteCongrats to him and all the best.
Hongera sana Dr Harun, umeonyesha njia njema kwa vijana wa kitanzania.
ReplyDeleteTuwache kulalamika na kushabikia siasa tufanye kazi na sisi tupate kutambuliwa kimataifa.
Hongera daktari kwa kutambuliwa kimataifa kutokana na utafiti wako wa kiwango, tunakutakia mafanikio katika kufanikisha matibabu ya moyo kitaifa na kimataifa. Hongera sana.
ReplyDeleteHongera sana Dr. Nyagori kwa kazi nzuri. Hivi Dr. Janabi alipataga tuzo au alipata utambuzi wa namna gani kimataifa? Nadhani sasa tuna madaktari wawili bingwa wanaotambuliwa kimataifa.
ReplyDeleteHongereni sana. Kwa mwenye kumbukumbu naomba anikumbushe recognition ya Dr. Janabi ilikuwa ya kitu gani nadhani miaka 3 au 4 imesihapita.
Madaktari wengine endelezeni jitihada zenu. Nimekumbuka pia kuwa.Dr..Makani naye alitambuliwa Kimataifa. Hivyo watanzania tunasonga mbele kwenye fani ya utabibu.
Hongera sana Dr.Nyagori umetoa fundisho kwa watanzania. Mungu azidi kukuinua....we are proud of you.
ReplyDeleteDokta umetisha yani hongera mnoo naamini watanzania watakua na chakujifunza kupitia wewe..BRAVO!! We are proud of you.
ReplyDeleteHongera xana. Am happy for you
ReplyDeleteHongera sana Dr. kwa kazi nzuri na kwa kulitangaza vizuri jina la nchi yetu.
ReplyDeleteDr. Hongera mno mno kwahatuahyo uliyopiga kwani itafungua milango kwa madaktari wengine hapa Tanzania kushiri kwenye tafti mbalimbali duniani kote
ReplyDelete