Kundi linaloundwa na wasanii wa filamu,wanamuziki na wanamichezo kwa ajili ya kusukuma gurudumu la  maendeleo yao na taifa kiujumla la Friends of Developments(F.O.D), limepania kufanya mengi makubwa kulisimamia jina lao la “Rafiki wa Maendeleo” kwa kufanya kazi za kijamii zikiwemo kusaidia wasiojiweza, kwa kujitolea na kufanya matamasha mbalimbali mfululizo na hasa kipindi hiki cha uchaguzi.

Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa FOD na pia katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini IBRAHIM KAMWE “Bigright” amesema – FOD inayoongozwa na Rashid Nasor “chidy mzee wa mbele” recho na Crama tayari imeshajikusanyia wanachama zaidi ya milioni tatu  wengi wakiwemo,wanafunzi wa vyuo,  viongozi wa chama na serikali wazee kwa vijana.

Kwa kuwa FOD yenyewe ina simamia zaidi maendeleo , na kipindi hiki ni cha uchaguzi  ikaweka muswada wa kumsapoti kiongozi wanayeona atawaletea maendeleo na ambaye tayari amekwisha fanya mengi yaliyoonekana ambaye ni John Pombe Magufuli.

FOD  imedhamiria kwa dhati itajituma kila kona ya Tanzania kuhakikisha magufuli anakuwa madarakani washirikiane nae katika kulisukuma hilo gurudumu la kuleta maendeleo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...