
Na
Mwandishi Wetu
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) imetangaza orodha ya waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao
fomu za maombi zimegundulika kuwa na upungufu na kuwataka kufanya marekebisho
kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi
hiyo leo (Ijumaa, Agosti 28, 2015), jumla ya fomu za waombaji wa mikopo 7,788
kati ya 68,445 zilizopokelewa na kuhakikiwa zimegundulika kuwa fomu zina upungufu
na kuwataka waombaji kusoma majina yao katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega, (Pichani) waombaji ambao fomu zao
zimegundulika kuwa na upungufu wanatakiwa kurekebisha kabla au ifikapo tarehe
11 Septemba mwaka huu (2015).
“Baada ya kusitisha uombaji wa mikopo kwa
njia ya mtandao kwa mwaka wa masomo 2015/2016, Bodi ilianza kufanya uchambuzi
wa maombi yote yaliyopokelewa na kugundua kuwa maombi 7,788 ya mikopo yanakosa
taarifa muhimu,” inasomeka taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa
hiyo, taarifa muhimu zinazokosekana ni pamoja na sahihi za waombaji, nakala za
vyeti vya kuzaliwa vya waombaji, sahihi na picha za wadhamini na baadhi ya fomu
za maombi kutosainiwa na wanasheria na maafisa wa serikali za mitaa kama
maelekezo yanavyotaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...