Na Lorietha Laurence- Maelezo

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja  Ndege nchini (TAA)  Bw Suleiman Suleiman  ametoa ufafanuzi kuhusu hitilafu ya umeme iliyotokea katika uwanja wa ndege wa Mwanza kuwa imetokana na marekebisho ya kangavuke (generator) ya dhalura katika uwanja huo.

Bw. Suleiman ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii na kuongeza kuwa kila kiwanja cha ndege nchini kina generator ya dhalura.

“Viwanja vyote vya ndege nchini vina generator za dhalura, lakini kwa upande wa Mwanza hivi karibuni, generator hiyo ilipata tatizo la kiufundi na taarifa ilitolewa kwa makampuni yote ya usafirishaji wa abiria wanaotumia uwanja huo” alisema Bw. Suleiman.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, mamlaka imeshafanya utaratibu wa kununua generator mpya itakayofungwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza wakati wowote kuanzia sasa kutatua tatizo hilo.

Aidha Mkurugenzi huyo wa TAA nchini ameeleza kuwa pamoja na tatizo la kukatika umeme katika uwanja wa ndege wa Mwanza, hali ya usalama katika uwanja huo pamoja na viwanja vingine nchini iko vizuri.

“Pamoja na tatizo hili, nawahakikishia wasafiri wanaotumia viwanja vya ndege nchini na watanzania kwa ujumla kuwa hali ya usalama katika viwanja vyetu imethibitiwa,” amesema.

Tanzania ilishika nafasi ya pili mwaka 1999 ilipokaguliwa na shirika la usalama wa usafiri wa Anga Duniani ambayo hufanya ukaguzi kwa wananchama kuhakikisha kuwa nchi wanachama wanafikia vigezo. Shirika hilo linatarajia kufanya ukaguzi mwezi Septemba mwaka huu.

Hivi karibuni abiria wa kwenda Mwanza kupitia kampuni ya usafirishaji ya Fastjet walihairishiwa safari zao kutokana na hitilafu ya umeme katika viwanja vya ndege vya Mwanza ambao ulikuwa ukifanyiwa matengenezo tangu ijumaa iliyopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hiyo generator inunuliwe kwa haraka iwezekanavyo, si vizuri kukosa umeme wa dhararura katika kiwanja kama cha Mwanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...