Tunapoelekea kwenye kipindi hiki cha uchaguzi wagombea urais watarajiwa wanajaribu kuwaeleza watu  mambo yenye mvuto kwao na kuonyesha  kuwa wataifanya Tanzania  iwe nchi ya maziwa na asali. Nafahamu watatupa ahadi nyingi zaidi wakati wa kampeni.
Lakini kinachonisikitisha  zaidi ni pale  wanasiasa  wanaposema  wanakerwa na umaskini wa watanzania na nia yao  ni kuondoa umaskini. 
Lakini hapo hapo anahamasisha maelfu ya  vijana na watu wengine kuacha kazi zao   kumsindikiza kwenda kuchukua fomu ya uteuzi na kuwafanya waache shughuli zao kwa siku nzima, wamesimamisha shughuli za kiuchumi mjini kwa zaidi ya masaa matano nk.  
Je kwa kufanya hivyo tumeongeza  umaskini au tumepunguza umaskini wa mtanzania?. kama kweli tunajali watanzania na tunataka kuwaondolea umaskini kwanini usiende kuchukua  fomu na viongozi na washabiki wako wachache   halafu uongee na watanzania kupitia vyombo vya habari. 
Hawa waheshimiwa wanajua ni kiasi gani cha pesa kimepotea kwa wao kufunga barabara na shughuli zote mjini kwa zaidi ya masaa matano. je wanajua hawa maelfu ya vijana na watu wengine waliokusanywa na kuandamana kwa siku nzima  kumsidikiza mgombea wamepoteza kipato kiasi gani?

 Naomba watanzania   kipindi hiki cha uchaguzi   tusikitumie  kuongeza umaskini na kutegemea  viongozi wetu watuondolee umaskini wakiingia  madarakani. Umaskini inabidi tujiondolee wenyewe. 
Kuna tafiti zilionyesha kiasi cha fedha kinachopotea kutokana na  foleni za magari  jijjini Dar es Salaam, watu kukaa muda mrefu barabarani na kuchelewa makazini. Ningefurahi kama wasomi wetu wangefanya utafiti na kubainisha  kiasi gani cha fedha kinachopotea kwa kusimamisha  shughuli za uchumi kwa misafara  isiyo na muhimu kama kusindikiza wanasiasa kwenda kuchukua  fomu za uchaguzi.


R. Kahwa  - Mtanzania 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. The mdudu, mimi nilikua mfuasi wa CCM toka utotoni nikatoka baada ya maoni ya wanachi kucha kachuliwa nimejiunga na UKAWA hawa nao wamenizingua baada ya mauza uza yao ndio nikachukua muda wangu kuipigia macho ACT Wazalendo na baada ya kugundua kuna AZIMIO LA TABORA na la ARUSHA inayohusiana na miiko ya uongozi bila kinyongo wala wasiwasi nikajiunga na ACT Wazalendo so mimi sipo kabisa na mambo ya CCM na UKAWA coz hata wakishinda ni sawa sawa na bule kabisa na mkae mkijua ndugu zangu watanzania wezangu CCM na UKAWA wote hawana miiko ya uongozi so msitegemee mapya toka kwao.

    ReplyDelete
  2. Kweli ndugu sidhani kama hii ni Hoja hata kidogo kwani haina mashiko, Hiki ni kipindi kinachokaribia uchaguzi, hata kama Kampeni za uchaguzi hazijaanza rasmi ni kipindi ambacho wanasiasa wanakisubiri kwa muda mrefu na kinatokea kila baada ya miaka mitano. Na kikipita inabidi kila mtu(mwanasiasa) arudi kwenye kambi yake na kusubiri miaka mingine mitano.
    Sidhani ni dhambi kubwa sana kama unavyodhania kwa mwanasiasa kukitumia kipindi hiki kuhamasisha wanachama na wapenzi wake kwenda kuchukua fomu ya uraisi na kuwaondoa watu katika shughuli zao za uzalishaji mali za kila siku kwani uongozi wa ngazi zote ktk Nchi unamhusu mtu moja moja katika maisha ya kila siku. Na ishitoshe nadhani wewe ni mkereketwa wa CCM na umejisikia vibaya Lowasa kupata wasindikizaji wengi kwenda kuchukua Fomu, Labda kwa haraka-haraka nikuambie kuwa wasindikizaji wengi walikuwa ni vijana na asilimia kubwa ni vijana wasiokuwa na kazi au shughuli maalum na wamepata muamko mkubwa wa mabadiliko baada ya chama chako tawala kuwanyima Fursa za Elimu na Ajira na wamejitokeza kwa wingi vile ili kukudhihirishia kwamba wamechoka na maisha haya.

    ReplyDelete
  3. Kwani ccm hawa kufanya hivyo majuzi. Usiwe na maono hasi hivyo

    ReplyDelete
  4. Ndugu maoni yako hayana mashiko hata chembe. unasahau kuwa hiki ni kipindicha uchaguzi na vijana wamehamasika kutumia haki yao ya kikatiba. wanao uhuru wa kumsindikiza mgombea wanayempenda na kumshabikia pia. CCM walipokusanya vijana na wanachama wao kumsindikiza mgombea wao hukutoa neno lakini kwa kuwa umedhamiria kuwapotosha wapiga kura umetumia gia ya umasikini.

    ReplyDelete
  5. wajibu wa kuondoa umasikini ni wetu wote viongozi wa ngazi zote wanatakiwa kutuhamasisha na kutuwezesha katika hilo. Malengo yaliyopimwa ya kuongeza vipato, kuondokana na mipango na kilimo kisicho na tija, makazi duni yaliyopitwa na wakati, na kuhakikisha huduma za umeme maji zimemfikia kila mtanzania katika kipindi kifupi cha miaka mitano malengo haya yanawezekana. Jinsi tunavyobaki nyuma ndiyo tunazuia ongezeko la mapato ya maeneo yetu na taifa kwa ujumla.

    ReplyDelete
  6. Waandishi wa habari kama huna chakuandika kinachoweza kumuelimisha mwananchi tafadhali kaakimya siodhambi kabisa ushabiki wa kuandika maelezo yanayo kandamiza hisia zawatu wengine sio sahihi ccm walipo msingikiza mgombea wao hatukuona hoja hizi sasa kaeni kimya mwananchi ndio mwenye maamuzi ya akitakacho jua yako kama huna mawazo mema sijaona kiongozi yoyote aliyeenda mahali akaacha kupokelewa au kusindizwa ww nimbea wa ccm Watanzania wenye uchungu na nchi yao tunaomba mungu awape upofu waandishi wapotoshao uma.

    ReplyDelete
  7. Watanzania sasa hivi chagueni Mtu ambaye yuko makini na sio chama chagua kila mahali ambapo unaona huyo mtu anatufaa bila kujali yuko chama gani mcha Mungu, mwenye mapaji saba ya roho mtakatifu 1.Hekima 2.Akili, 3.Elimu 4.Shauri 5.Nguvu 6 Ibada 7.Uchaji wa Mungu akiwa na hivyo vyote hawezi kuwa na Ubinafsi, udini wala ukabila, kwani Ubinafsi, Udini na ukabila ndio mambo yanayoleta ubaguzi na utengano katika jamii kupelekea watu kukata tamaa. Watu wenye hekima wapo na mtu akiwa na hekima ataipeleka nchi mahali pazuri

    ReplyDelete
  8. Je watapiga kura? au ndio ushabiki tu maana navyojua bongo kwa ushabiki namba moja vitendo namba ziro..

    Mdau hapa.

    Deutschland

    ReplyDelete
  9. Mnatoa wapi mawazo ya kuondoa umasikini? Ni nani kawaambia kuwa umasikini unaondolewa?

    Tunaweza kupunguza umasikini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...