Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin wakati alipowasili hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo kuhudhuria hafla ya Kongamano la pili la Diaspora. Kushoto mwenye kanzu ni Mhe Ali Mzee Ali, Mjumbe wa Bodi ya AICC
Rais Kikwete akiwa meza kuu na viongozi wengine katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo wakati wa hafla ya Kongamano la pili la Diaspora. Wengine kutoka kulia ni Mhe Ali Mzee Ali, Mjumbe wa Bodi ya AICC, Bw. Matheu Lamolle Mtafiti wa Massoko wa Taasisi ya International Trade Centre (ITC) ya Uswisi ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa kongamano hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar (Utawala Bora) Mhe Dk Mwinyihaji Makame, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania DMV Marekani Bw. Iddi Sandaly, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula na Bi Mariam Mungula wa Diapora London
MC wa hafla hiyo ambaye ni Mratibu wa Dawati la Diaspora katika Ofisi ya Waziri Mkuu Bi Suzana Mzee akiwa kazini
Wadau wa Diaspora kutoka nchi mbalimbali na Tanzania katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo wakati wa hafla ya Kongamano la pili la Diaspora.
Inapendeza sana kuona diaspora na SMEs wapo makini katika kuchangia uchumi wa nchi yetu.
ReplyDeleteIla nasumbuka kidogo kufungua kuangalia picha zaidi. Michuzi hamna tatizo lolote la kiufundi?
link haifanyi kazi
ReplyDeleteDiaspora wanachangia uchumi wetu sawa. Uraia nchi mbili hapana. Wenzetu hawa walidhiriki kuuu-kana utaifa wao ili wapate maisha mazuri huko ughaibuni... Leo hii wana uchungu wa kutaka kuwa wa-tanzania? Napita tuuu
ReplyDeleteJe,kuna incentives zozote Diaspora wanapata katika kuwekeza nyumbani? i.e on taxes, duties etc
ReplyDelete