Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwasalimia baadhi ya Wanawake wanaounda Baraza la Wanawake wa Chadema, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Jengo la LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam, wakati walipowasili kwa kuhutubia Baraza hilo.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza machache wakati akiwasalimia maelfu ya Wanawake wanaounda Baraza la BAWACHA, waliokuwa wamekaa nje ya jengo la LAPF kutokana na kukosa nafasi ndani ya Ukumbi huo. Mh. Lowassa alilazimika kusimama na kuwasalimia kinamama hao kabla ya kuingia Ukumbini kulihutubia Baraza hilo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimueleza jambo, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA), Mh. Halima Mdee wakati akilihutubia Baraza hilo.

KUONA PICHA ZAIDI

BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sura nyingi ni za kutoka kulekule sioni za pwani mbona mnalazimisha kwenda ikulu WHY? basi huo Ukakasi wenu oops sorry Ukawa wenu mngekuwa basi mnafanya na mambo ya kimaendeleo japo tuyaone machoni mwetu hakuna hata moja mnalolifanya zaidi ya KUANDAMANA JUU YA BARABARA ZA MAGUFULI ni mimi wenu muona mbali @team magufuli#hapakazitu watu gani msiokua na SHUKURANI nyie? mtapofuka macho mungu yupo Mjomba Michuzi sambaza upupu wangu ili wajikune

    ReplyDelete
  2. Jamani leo Halima Mdee mnyenyekevu kweli kwa mtu aliyekuwa anadai ni fisadi namba moja!! Kweli hujafa hujaumbika!!!

    ReplyDelete
  3. Yaani, Chadema tumechelewa kiasi kwa dada mdogo Halima Mdee kutukumbusha kuwa tumesahau akina mama?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...