Wanachama wa chama cha ADC wakishangilia mara baada ya kumtangaza mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar katika mkutano wa kamati kuu uliofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa chama cha ADC wakipata burudani kutoka kwa kijana wao wa burudani katika mkutano mkuu wa chama hicho wa kumtangaza mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,mgombea urais wa Zanzibar na mgombea mweza katika nafasi hiyo, katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Katibu mkuu wa chama cha ADC, Lydia Bendela akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha ADC ambao walikuwa wanawatangaza wagombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na wa Zanzibar pamoja na Mgomea mweza katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chifu Lutalosa Yemba anayegombea nafasi ya Urais kupitia chama cha ADC akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwania nafasi hiyo leo katika mkutano wa Kamati kuu wa chama cha ADC uliofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa chama cha ADC Said Miraji Abdallah akizungumza mara baada ya kutangazwa kugombea nafasi ya kuwa mgombea mweza kupitia chama hicho leo katika mkutano wa kamati kuu uliofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADC, Chifu Lutalosa Yemba na Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed wakipunga bendera za chama chao kuashiria ushindi wa kuwania nafasi za juu uongozi katika chama hicho, katika mkutano wa Kamati kuu uliofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Blogu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...