Na Mwandishi Wetu ,
KUTOKEA kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani
kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na
maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki.
Takriban watoto 8
kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu
hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa
takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani
Afrika inaweza kuwa wengi sana.
Watoto
wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati wa kuzaliwa.
baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa bluu,
mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo,
kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto
kupata maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...