Wizara ya Nishati na Madini inaendelea na mpango wake wa Mafunzo kwa Wachimbaji Madini Nchini kuhusu matumizi ya Mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya Mtandao yaani Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP).
Pamoja na malengo mengine, Mfumo huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za Serikali ziwe zinapokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima ili kuwajengea uwezo.
Baadhi
ya wachimbaji Madini wa Songea wakimsikiliza Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati
na Madini (hayupo pichani) wakati wa mafunzo hayo ya Mjini Songea
Mtaalamu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idd Mganga akiendelea na mafunzo hayo kwenye
ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Ufundi (VETA), mjini Songea.
Afisa
Madini Mkazi Tunduru, Mhandisi Frederick Mwanjisi akifungua mafunzo hayo kwa
wachimbaji madini yaliyofanyikia katika ukumbi wa Clasta wilayani Tunduru.
Wataalamu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakiwaelekeza wachimbaji wadogo wa wilayani
Tunduru namna Mfumo wa Huduma ya Leseni kwa njia ya Mtandao unavyofanya kazi.
Wa Kwanza kushoto ni Idd Mganga na anayemfuatia ni Mhandisi Edward Mumba.
Mchimbaji
mdogo wa Wilayani Tunduru, Mwajuma Omari akitoa shukrani kwa niaba ya
wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo hayo kwa Wataalamu kutoka Wizara ya
Nishati na Madini hawapo pichani.
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini- Kitengo cha Leseni, Idd Mganga (kushoto aliyesimama) akielezea Historia ya utoaji Leseni za Madini nchini wakati wa Mafunzo kwa Wachimbaji Madini Songea. Wa kwanza kulia ni Mtaalamu kutoka Kitengo hicho, Mhandisi Edward Mumba na anayemfuatia ni Mhandisi George Wandibha wa Ofisi ya Kanda ya Madini Songea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...