Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais mara baada ya kuchukua kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam leo, ambapo walisindikizwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamepanda kwenye gari maalum.

Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza
Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha mkoba wenye fomu za Kuwania Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho mbele ya wananchi
na wanachama wao nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar
es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea
Urais leo agosti 4, 2015.
Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na
Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt
John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Urais kupitia
chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwashukuru Wananchi na wafuasi
wa chama cha CCM walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John
Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Urais kupitia chama
hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
Mhe
Samia Suluhu Hassan akiwashukuru Wananchi na Wanachama wa CCM
waliojitokeza kwa wingi nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini
Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za
kugombea Urais leo agosti 4, 2015.
Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza
Mhe Samia Suluhu Hassan nwakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM
Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi
kuchukua Fomu za kugombea Urais leo agosti 4, 2015.
Picha ya pamoja
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi
Taifa Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam,Ndugu Ramadhan
Madabiba pamoja na pichani shoto Ndugu Januari Makamba aliyeshinda kura
za maoni CCM jimbo la Bumbuli kwa pamoja wakimsindikiza Dkt Jonh Pombe
Magufuli kuchukua fomu za kuwania Urais mapema leo jijini Dar.
Wafuasi
wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi Ndogo ya Makao
ya CCM mtaa Lumbumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais
kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua
Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Tunawatakia ushindi mkubwa na mafanikio mtakapoanza kampeni ya nchi nzima.
ReplyDelete
ReplyDeleteJPM FOR PRESIDENT !
CCM HAPA MMEWAPIGA BAO WAPINZANI! TUMEUONA UTENDAJI WAKO KIONGOZI.
HUO UMATI MKUBWA HAKUNA MICHUZI LINE, IT IS GENUINE.
"CHAMA TAWALA" DODOMA BIG UP. MNGEVURUNDA KWENYE KUMPATA HUYO MNGETUANGUSHA WATZ WENYE LOGICAL THINKING.
YOU GAVE US THE MOST SUITABLE, 'CLEAN', ETHICAL, WITH A CONSTRUCTIVE BRUTAL DRIVE.
I ONCE HEARD THIS, AND I WAS DISSAPOINTED ON THAT REASONONG. ETI MKALI!
CCM mtashinda bila wasi wasi .All the best
ReplyDeleteBrother Michuzi unaweza kutuwekea video ya hii event kama unayo? Tulio mbali tunafarijika kusikia walichosema hawa watarajiwa
ReplyDeleteCCM Mwaka huu mmefanya uchaguzi ambao watz hawakutarajia, mmeonesha kuwa fedha si kigezo cha kumpata mtu anayestahili kuongoza, bali ueledi, ujuzi, umahiri na uwezo wa kuchapa kazi ndio kipaumbele cha mgombea anayetakiwa.
ReplyDeleteBig up sana, all the best Hon. Magufuli