Dkt John Pombe Magufuli kwa pamoja akicheza wimbo wa Adinselema uliokuwa ukiimbwa na wanachama hao mara baada ya kumpokea na kuamsha shamra shamra na shangwe za hapa na pale.Pichani kulia ni Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akishuhudia.
Mgombea Uraisi wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na shamra shamra kutoka kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM waliokuwa wamekusanyika nje ya ofisi za CCM mkoa wa Lindi,alipofika kusaini vitabu,kuwashukuru na kujitamulisha kwao.

Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akizungumza jambo na Wanachama wa chama hicho nje ya Ofisi za CCM mkoa wa Lindi
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM na wafuasi wa chama hicho waliofika kumlaki alipowasili kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama hao mapema leo Agosti 8 2015.Dkt Magufuli amewataka wananchama hao kushikamana kuwa wamoja katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi,ambacho anaamini kitaipatia ushindi chama cha CCM.
Dkt John Pombe Magufuli akitia sahihi vitabu ndani ya ofisi ya CCM mkoa wa Lindi,pichani kati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa,Ndugu Ali Mtopa pamoja na
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi,Ndugu Ali Mtopa alipowasili  kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM mkoani humo mapema leo Agosti 8 2015.

PICHA NA MICHUZI JR-LINDI

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hawana umri wa kustaafu (kung'atuka)ili kuendana na wakati (mambo ya sayansi na teknolojia,internet, laptop, nk)??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...