Na Bashir Yakub.
Kumekuwepo na sintofahamu nyingi kwa madereva na watumiaji wengine wa vyombo vya usafiri. Sintofahamu hii imekuwa ikiletwa na baadhi ya mambo ambayo hayaeleweki sawasawa katika suala zima la usalama barabarani na sheria zake. Wadau wa barabarani wamekuwa wakilaumiana, madereva wakiwalaumu askari wa barabarani kwa uonevu huku askari wa barabarani wakiwalaumu madereva kwa ukorofi na ukosefu wa utii wa sheria bila shuruti. Lakini swali hapa ni kwanini iwepo mivutano na hali kuna sheria. Sheria inasemaje kwa kila jambo ambalo wadau hawa wanatofautiana?.
1.UBABE WA ASKARI WA BARABARANI.
Baadhi ya askari wa barabarani wamekuwa ni wababe sana. Wanahoji mambo ambayo si wajibu wao kuyahoji na hawataki dereva aulize lolote kuhusu kuhoji kwao mambo hayo. Wanataka kila wanachosema dereva atii hata kama anaona hakipo kwa mujibu wa sheria. Matokeo yake mtu anaandikiwa faini za makosa mengi ilimradi tu kumkomoa. Askari wengine wamefikia hatua ya kuwapiga madereva vibao. Binafsi nimewahi kushuhudia askari wa usalama barabarani akimnasa kibao dereva wa daladala. Ni ubabe uliovuka mipaka na hakika ni uvunjaji wa sheria uliopitiliza .
2. JE TRAFIKI ANARUHUSIWA KUMNYANGANYA DEREVA LESENI.
Masuala ya usalama barabarani yanaainishwa ndani ya Sheria ya Usalama barabarani ( The Road Traffic Act) ambayo ndio hueleza wajibu na haki za kila mdau na mtumiaji wa barabara. Katika sheria hii hakuna pahala pameandikwa kuwa trafiki achukue leseni ya dereva kwa kuwa dereva ametenda kosa fulani. Maana fupi ya hili ni kuwa trafiki haruhusiwi kuchukua leseni ya dereva. Anachoweza kufanya trafiki ni kile kilichoainishwa na kifungu cha 17 cha sheria hiyo ya usalama barabarani. Kifungu hicho kinampa trafiki mamlaka ya kukagua na kujiridhisha na uhalali wa leseni ya dereva. Hakisemi aichukue. Kinasema aikague basi. Kukagua na kuchukua ni mambo mawili tofauti.
Kama hivyo ndivyo basi yafaa kueleweka kuwa kitendo cha askari kumsimamisha dereva na kisha kumpokonya leseni yake ni kinyume cha sheria. Dereva anao wajibu wa kulinda haki hii kwa kulikataa hili na kuhakikisha trafiki hamfanyii kitendo hiki. Kumbuka kuwa wakati askari wa barabarani akitekeleza wajibu wake wa kisheria na wewe dereva unayo haki ya kutetea haki zako za kisheria. Hakuna aliye juu ya mwingine kwani anatekeleza wajibu nawe unalinda haki.
Hii ni kweli kabisa...traffic polisi wanaharibu jina la tz..mimi pia waliwahi kunikamata bila kosa..baada ya kumuuliza yeye ni nani akasema swali gani hilo huoni kama nimevaa uniform..nikamwambia naona umevaa nguo nyeupe lakini sioni namba zako za kazi akaja juu namba utaziona kwenye karatasi za kwenye sharti nitakuwa nimedondosha...nikamwambia za kuandika kwenye karatasi hata mimi naweza kuandika....kwahiyo utani dhibitishaje kama wewe ni trafic polisi akawa mbogo nikamwambia usinifokee mi sio mwanao...wakaja na wenzake wengine wakanaza kuniambia wewe dada mkorofi nikawauliza kuuliza namba za polisi ndio ukorofi mwanamke trafic akanijibu utamuulizaje polisi...nikamwambia zamani wakati tulikuwa gizani ndio yulikuwa hatuuulizi ...wacha wafoke wote twende kituoni...nikwaambia twendeni mara eti wapande gari langu nikawaambia hakuna nafasi nikasumbuana nao sana hatimaye tukaenda kituoni...kufika huko boss hayupo jamaa tuliemkuta hapo kalewa balaa na uniform zake mbona majanga tunasafari ndefu sana ya kuelimishana...hilo halikunipa tabu mimi niliona ni challenge nzuri sana sikunyingine hata onea watu ....lakini wazungu wageni wanapata tabu saaana na hao trafic kiasi kwamba wakirudi makwao wanaweka kwenye holiday review zao na jina la tz linaharibika kwa sababu ya wachache wasio thamini kazi zao na nchi yao wanaangalia maslahi yao tu...hawa polisI wanatakiwa kuelimishwa na kufahamishwa umuhimu wa watalii ktk nchi yao..sio wanaona ni wazungu basi wanawaona wajinga au hawajui kitu hao au hawajui kiswahili wanatumia nafasi hiyo kuharibu jina la tz
ReplyDelete