Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amesema wakati sasa umefika kwa wasanii kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, badala ya kuendelea kuchangishana fedha za matibabu kila wanapougua.
Amesema kutokana na kupanda kwa gharama za maisha hivi sasa zikiwemo za matibabu, wasaani wana kila sababu ya kuona umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili wanapougua watibiwe kwa kutumia kadi badala ya kuhangaika kutafuta fedha taslimu.
Makonda alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kuhusu huduma za matibabu kupitia mpango maalumu wa bima ya afya kwa wajasiliamali na vikundi vilivyosajiliwa unaojulikana kama KIKOA.
Amesema hivi sasa wasanii wengi wanahangaika kupata matibabu katika mazingira yasiyoridhisha kwa kuwa hawana bima za afya hivyo ni muhimu kwao wachangamke fursa hiyo ambayo itawawezesha kuchangia kabla ya kuugua na hivyo kuwa na uhakika wa kutibiwa hata kama hawana fedha mfukoni.
Naye Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Eugen Mikongoti amesema NHIF imeanzisha utaratibu huo wa kuchangia kwa kundi la wajasiliamali ili kuwapa uhakika wa matibabu wakati wote wanapokua katika shughuli zao za kuelimisha na kuhamasisha jamii katika masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Amesema kwa kuchangia 76,800 mwanachama wa KIKOA atakuwa na uhakika wa kutibiwa mwaka mzima katika vituo vya matibabu zaidi ya 6000 vilivyosajiliwa na Mfuko nchini nzima.
Mikongoti amesema NHIF itawatumia wasanii hao katika kuelimisha umma ili kuhakikisha kuwa ujumbe wa umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaenea nchini nzima.
Katika semina hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Baraza la Wasanii Tanzania (BASATA), viongozi wanne wa Shirikisho la Wasanii walikabidhiwa kadi zao za bima ya afya zinazowawezesha kupata matibabu wakati wowote watakapougua.
Mpango wa bima ya afya kwa wajasiliamali – KIKOA- unawalenga wajasiliamali walio katika vikundi vilivyosajiliwa, ambapo hadi sasa zaidi ya vikundi mia moja vyenye wanachama zaidi ya elfu ishirini vimejiunga na Bima ya Afya.
Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni, Paul Makonda akihutubia wasanii juu ya kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo Jiji Dar es Salaam.

Mkurungezi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Eugene Mkongoti akizungumza na wasanii juu ya Mpango wa bima ya afya kwa wajasiliamali – KIKOA- unawalenga wajasiliamali walio katika vikundi vilivyosajiliwa, Katika semina hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Baraza la Wasanii Tanzania (BASATA).
Baadhi ya wasanii wakifuatilia mada.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...