Marafiki wa Wafanye Watabasamu, hivi karibuni, walitembelea kituo cha watoto yatima (Amani Orphanage Centre) kilicho katika Kijiji cha Zinga, Bagamoyo kwa ajili ya kutoa misaada mbali mbali kisha kuchora nao. Mbali na marafiki waishio nchini, pia kulikuwa na walimu sita toka Shule ya Msingi ya Catton Grove ya Uingereza na wawakilishi wa taasisi ya The Tanzania Norwich Association pia ya Uingereza. (Picha: Nicolas Calvin).
Msafara wa Wafanye Watabasamu ukiwasili kituoni hapo. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu.
Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Centre, Bi. Margareth Mwegalawa wa pili toka kulia aliyesimama, akitoa taarifa fupi kuhusu kituo hiko.
Mratibu wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni mchora vibonzo ITV, Nathan Mpangala akiwashukuru marafiki mbalimbali waliochangia misaada na kufanikisha ziara hiyo.
Sanaa ya uchoraji nayo ikachukua nafasi yake.
Baadhi ya watoto na marafiki wa Wafanye Watabasamu wakionesha kazi zao.
Naam, raha ya shughuli mlo bwana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mkuu naomba mawasiliano ya hiki kituo na mimi nataka nikawatembelee hawa watoto pia.

    ReplyDelete
  2. mpe huyu jamaa contacts za kituo kingine ambacho hakina wafadhili, kama unataka contact just Google them.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...