![]() |
Marehemu Mzee SK George Mallya |
Familia ya Mallya inasikitika kutangaza kifo cha Mzee SK George Mallya aliyefariki kwenye hospitali ya KCMC siku ya Jumamosi tarehe 8 Agosti. Taarifa ya familia inaeleza kuwa marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamisi tarehe 13 Agosti, nyumbani kwake Maili-Sita, Moshi, ambako mipango ya mazishi inafanywa kwa sasa.
Marehemu Mzee SK George Mallya atakumbukwa kama mmoja wa wanajeshi shupavu wa Kings African Rifles (KAR) wa Tanganyika Battalion nyakati za Vita Kuu vya Pili (World War Two) ambapo alienda kupigana na Wajapani kule Burma (siku hizi Myanmar).
Baada ya Vita kuisha mwaka wa 1945, alishika nyadhifa mbalimbali katika Serikali za Mitaa, hadi kuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Kiafrika wa Jiji la Dar es Salaam. Baada ya kutoka Serikalini, aliiongoza kampuni ya Lonrho Tanzania hadi alipostaafu na kuhamia Moshi.
Ameacha watoto wanne wa kike na mmoja wa kiume, pamoja na wajukuu na vitukuu kadhaa.
Mungu Ailaze Roho yake
mahala pema Peponi.
mahala pema Peponi.
AMINA
RIP Mzee Mallya mchango wako mkubwa katika nchi hii tumeutambua.
ReplyDeleteRIP Mzee Mallya
ReplyDelete