Na.Aron Msigwa - MAELEZO,ARUSHA
Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali yamepunguza upotevu wa mapato uliokuwa ukisababishwa na watendaji wasio waaminifu.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Arusha na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Adorf Mapunda wakati akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali Mtandao uliowahusisha maafisa TEHAMA,Rasilimali watu,Utawala na Maafisa Habari kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Amesema mabadiliko hayo ya ukusanyaji wa fedha kielektroniki yameongeza ufanisi kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuondoa wizi na vitendo vya rushwa vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu.
Ameeleza kuwa utendaji wa Serikali na taasisi zake umerahisishwa kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Bw.Adorf Mapunda akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali mtandao kwa Maafisa TEHAMA,Rasilimali Watu,Utawala na Maafisa habari kutoka maeneo mbalimbali nchini jana jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...