Mashua zenye tanga zinazojaza upepo zikichanja mbuga katika mawimbi makali kwenye bahari ya hindi kwenye fukwe za Yatch Club wakati wa mashindano ya mbio za Mashua za Mercedes Benz Cup 2015 yaliyodhaminiwa na kampuni ya CFAO Motors kwa miaka 9 sasa, yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
KLABU ya Yatch ya Dar es salaam iliyopo Msasani jijini Dar es salaam inatafuta fedha kuwezesha washiriki wake wanne katika mbio za mashua za kisasa kwenda kushiriki michezo ya All Africa games itakayofanyika baadae mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa patashika ya siku mbili ya mbio za mashua za kisasa zinazosukumwa na matanga yanayopokea upepo na zile ambazo hazina.
Mbio hizo ambazo zimedhaminiwa na CFAO Motors kupitia bidhaa yake ya Mercedes Benz Cup 2015 zilishirikisha watu 30 wakiwa ndani ya mashua 15 za aina tofauti.
Ofisa mmoja wa klabu hiyo Andrew Bogd alisema kwamba ushiriki wa watanzania katika mashindano ya kimataifa hautakuwa wa kwanza kwani wameshashiriki katika mchezo hiyo Afrika Kusini na Morocco mwaka jana.
Alikuwa akizungumzia mafanikio ya klabu hiyo katika kuufanya mchezo huo kujulikana kwa wazawa wa Tanzania ambao wanapenda michezo ya katika maji hasa ya kukimbiza mashua.
Katika mbio hizo ambapo kulikuwa na washindi takribani zaidi ya saba kwa kuzingatia daraja mshindi wa mashua zenye tanga inayojaza upepo alikuwa Al Bush akishirikiana na Robert Fine. Mshindi wa Pili wa ngazi hiyo alikuwa Michael Sulzer aliyekuwa katika mashua na Andreas Schmidt na ushindi wa tatu ulikwenda Roland Van de Ven akiwa na Peter Scheren.
Washiriki wakipambana na mawimbi wakati wa mashindano ya mbio za mashua za Mercedes Benz Cup 2015 yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...