Ankal,
Leo nimeshuhudia kitu kimoja ambacho hakikunipendeza hata kidogo na nimeona bora nikiongelee kwa vile ni hatarishi kwa mazingira yetu.
Picha hii inaonyesha mdada mwenye t-shirt ya kijani ambaye alikuwa anafanya usafi hapo kwenye maeneo ya junction ya AHM na Barak Obama roads. Wakati sisi tunasubiri kuitwa na trafiki kipindi cha asubuhi, nimemshuhudia dada huyo akisafisha na kuzisukumiza taka ndani ya huo mtaro wa pembeni.
Kwenye hizo takataka alizosukumiza ndani ya huo mtaro ilikuwepo na chupa ya plastiki ya nusu lita.
Sasa nikajiuliza huu ndiyo usafi gani? Huyu dada kweli amepewa maelekezo afanye hivi au ni uvivu wake wa kuzoa hizo taka taka?
Kwa maana hizo takataka zitabaki kwenye mtaro huo mpaka itakaponyesha mvua na ndiyo balaa la mafuriko litatokea. Na huu umeelekea ndiyo mtindo wake kwa hivyo hizo taka zitakuwa ni nyingi tu humo kwenye mtaro.
Nilitaka kumwambia kwamba hivyo anavyofanya siyo vizuri lakini akasonga mbele na sisi tukaitwa na trafiki na kuendelea na safari yetu.
Kampuni inayohusika na usafi tafadhali chukua hatua kuhusu hili, mueleweshe huyo dada kwamba hizo takataka zinatakiwa kuzolewa na siyo kutiwa kwenye mitaro kama anavyofanya yeye.
Mdau wa mazingira
Asante Ankal
ReplyDeleteTunashukuru kwa kutoa hii taarifa ni mwanzo wa kurekebisha tabia kama hiyo na pengine kuitokmeza kabisa.
ReplyDeleteTatizo hakuna sehemu ya kuzitupa hizo takataka,sisi watanzania ni matahira. pesa za kampeni ya Uraisi zipo tena nyingi tu lakini kununua vitendea kazi hakuna.
ReplyDeleteHii tabia wanayo wasafisha barabara wote. Jambo la kujiuliza hizi manispaa huwa zinawalipa hao kondurasi wa usafi wa barabara bila kukagua kazi iliyofanyika? Mitaro mingi kama si yote imejaa majani, mchanga na kila aina ya takataka, usafi wa mitaro pembezoni mwa barabara haupo kwenye hadidu rejea za kazi ya kusafisha barabara? Tafadhali tusemee kwa wahusika manispaa washuhulikie hili jambo ili kuondokana na adha ya mafuriko yasiyo na sababu kila mvua zikinyesha
ReplyDeleteShukran sana mdau, wewe utakua ni mbeba mabox umerudi likizo home au kimoja maana wala vumbi hawana tabia hii ya kufichua maumivu.. tembelea na kwenye mabank na ofisi za serikali ili ujionee customer services zilivyo balaa hapo bongo..
ReplyDeletemdau wa UK