Kikosi cha Timu ya Yanga, kikishangilia kwa pamoja ushindi wao mara baada ya Ngao ya Jamii yenye kuashiria kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, katika mtanange uliopigwa jioni hii dhidi ya Timu ya Azam, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imepata ushindi huo kwa mikwaju ya penati 8-7, baada ya dakika tisini za mchezo kumalizika bila kufungana.
Wachezaji wa Timu ya Yanga, wakishandilia ushindi wao huo pamoja na mashabiki wao wakuojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kushabikia timu yao iliyokuwa ikikipiga na Timu ya Azam. Yanga imepata ushindi huo kwa mikwaju ya penati 8-7, baada ya dakika tisini za mchezo kumalizika bila kufungana.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akiondoka na mpira mara baada ya kumpiga chenga ya mwili Beki wa Timu ya Azam, Pascal Wawa (aliekaa chini) wakati wa mtangange wa kuwania Ngao ya Jamii ya Ufungunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hakuna timu iliyoona lango la mwenzie mpaka dakika hii.
Kiungo machachari wa Azam, Farid Mussa akiangalia namna ya kumtoka, Geofrey Mwashiuya wa Yanga, wakati wa mtangange wa kuwania Ngao ya Jamii ya Ufungunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, hakuna timu iliyoona lango la mwenzie mpaka dakika hii.
Beki wa Azam, Pascal Wawa akionyesha umahiri wake wa kuondosha hatari langoni kwake mbele ya Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...