CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU MGOMBEA URAIS KUREJESHA FOMU



Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa baada ya hatua ya kuchukua fomu ya kuwania uteuzi wa ndani ya chama kugombea nafasi ya urais, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa kesho (LEO) Agosti 1, 2015 atarejesha fomu yake kwa ajili ya taratibu zingine za ndani ya chama.


Shughuli hiyo itafanyika kuanzia saa 9.00 jioni, ambapo mgombea atakabidhi fomu  yake Ofisi ya Katibu Mkuu, Makao Makuu ya Chama, Kinondoni, jijini Dar es Salaam katika hadhara ikayohudhuriwa na viongozi wa chama, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali.


Mheshimiwa Lowassa atarejesha fomu hiyo akiwa mgombea pekee baada ya kuwa ametimiza taratibu za kikatiba hususan kupata wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchi nzima.


Hatua hiyo ya kurejesha fomu itafuatiwa na taratibu zingine za kikatiba, ikiwa ni pamoja na vikao vya uteuzi ambavyo vitaketi kwa mujibu wa ratiba ambayo imeshapangwa na chama.



Imetolewa leo Julai 31, 2015 na;


Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano – CHADEMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...