Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa akiwapumbia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya leo Agosti 14, 2014. Mh. Lowassa na Mgombea mwenza wake Dkt. Juma Haji Duni, walikuwa jijini humo kwa ajili ya zoezi la kutafuta wadhamini wa Tume na kutambulishwa kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" akimueleza jambo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya leo Agosti 14, 2014.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dkt. Juma Haji Duni akiwahutubia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya leo Agosti 14, 2014.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe akipunga mkono pamoja na wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya leo Agosti 14, 2014.
KUONA PICHA ZAIDI
Ivi kuna haja ya kupiga kula jamani kwa hali hii???twaweza kutumia fedha za kampeni kwa mambo mengine na kuokoa muda......
ReplyDeleteDuh.....hahahahaha mie yangu macho, nimejiandaa kutazama watu wanavyotaka kuzuia maji ya mafuriko kwa mkono.....wengine ndio wameshaanza kutoa sheria na matamko ya ajabu ajabu.
ReplyDeleteHuo Uwanja wa Rwanda umekuwa maarufu sana ktk mikutano ya kisiasa na isiyo ya kisiasa. Kwa nini usijengwe vizuri na kuvutia zaidi? haifai kabisa ulivyo kwa mtazamo wangu. Anyway, hongereni sana kwa nyomi ya watu.
ReplyDeleteNA BADO HAPO HAJAENDA HUKO AMBAKO CCM IMEBOMOKABOMOKA, YAANI MWANZA,ARUSHA MOSHI. WATAKOMA.
ReplyDeleteUNAAMBIWA WATU WAMESHAAMUA, HATA KAMA LIPUMBA AND DR.SLAA WASIMAME NA KUANZA KURUSHA MAWE KWA UKAWA, WATU HAWA HAWATAELEWA KABISA NI KAMA WATAKUWA WANAMPIGIA MBUZI GITAA.
Uwingi wa watu sio kura nyinyi, ingekuwa hivyo kusingekuwapo na haja ya kupiga kura. Tukutane trh 25 oktoba, 2015.
ReplyDeleteAnkal hii inaongesha umehamia UKAWA rasmi..
ReplyDeleteYa Mola mengi. Tukubali tu yaishe maana.
ReplyDeleteHaijawahi tokea! Never seen before.Twaweza tumia maamuzi ya "wanaounga mkono waseme ndio na wasiounga mkono wasema sio" kuokoa rasilimali nyingi za Taifa.
ReplyDeleteHa....hivi huu wingi wa watu ndio kura zitakuwa hivi hivi? Wengi wao wanakwenda kumshangaa Lowassa tu na upendo wake wa madaraka. Ana lipi jipya la kuisema CCM? Kwa kuwa haikumchukulia hatua katika sakata la Richmond? Haya ndio malipo yake.
ReplyDeleteZoezi zima la uchaguzi na kanuni zake linatakiwa kwa watanzania wote walioomba nafasi ili wapewe nafasi sawa. Watu wanaweza kuhudhuria mikutano ya vyama vyote vinavyokuja kujinadi karibu yao lakini watachagua wanayemtaka na matokeo ya uchaguzi ndiyo yatakayohesabika mwezi wa kumi kufuatana na taratibu tulizojiwekea kama nchi.
ReplyDeleteLowasa na UKAWA ni kama nyerere na TANU..
ReplyDeletenyota ya lowasa yang'ara ..mungu amempa na atapata tuache fitina tutaenda motoni.. aliepewa kapewa. muhimu ni peace & love.. mungu ibariki Tanzania.
Umati wa Mrema au hata Slaa 2010 ilikuwa kama hii na tunaona matokeo yake. Hata kule Kenya Raila mikutano yake ilikuwa na watu wengi sana, lakin siku ya kupiga kura watu wakamchagua Uhuru.
ReplyDelete