Katibu tawala mkoa wa Arusha Ado Mapunda jana alizindua mashindano ya
kuibua vipaji vya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel
Rising Stars jijini Arusha na kuwataka vijana wanaoshiriki mashindano
hayo kujituma na kucheza kwa bidii ili kutimiza ndoto zao za kuwa
wachezaji nyota.
Hafla ya ufunguzi ilihudhuliwa na viongozi wa shirikisho la mpira wa
miguu nchini (TFF) mkoa wa Arusha, mdhamini wa mashindano Airtel
Tanzania na wadau wengine wa soka. Ufunguzi huo uliufanyika katika
uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
“Tumepewa nafasi ya kuwa washiriki katika mashindano haya ya Airtel
Rising Stars 2015. Hivyo inatupasa tudhihirishe kuwa mkoa wetu una
vipaji na tunaweza kuchangia katika maendeleo ya soka kwa kutoa
wachezaji kwenye timu za vijana za taifa”, alisema Mapunda
Arusha inashirikisha timu ya wasichana ambapo timu kombaini kutoka
mkoa huo itasafiri kuelekea Dar-es-Salaam mwezi ujao kushiriki
mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.
Timu nyingine kwa
upande wa wasichana ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya na Mwanza.
“Naamini vijana hawa wanaoibuliwa katika Airtel Rising Stars kila
mwaka wanahitajika sana katika kuongoza nchi yetu kufika mbali katika
Mafanikio”, alisema Mapunda na kuwapongeza Airtel katika kuwekeza
katika maendeleo ya Mpira.
Programu hii ya soka la vijana ilianzishwa nchini Tanzania na sehemu
nyingine barani Afrika mnamo mwaka 2011 na ime0nyesha kwa vitendo na
imekua chombo muhimu katika maendeleo ya soka hasa katika soka la
wasichana. Timu ya Taifa ya wasichana inaundwa na wachezaji kutoka
Airtel Rising Stars.
Alisema katika soka wachezaji wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira.
“ Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni
na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara
wanayopata”, alisema na kuwataka wasichana kuwa na malengo ya mbali.
Akiongea katika ufunguzi huo Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane
Matinde aliwashukuru viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu TFFA) na
chama cha soka mkoa wa Arusha kwa muda wao na ushirikiano wao katika
mashindano. “ Pia natoa shukrani zangu za dhati kwa mgini rasmi kuja
kuungana nasi katika uzinduzi huu.
Matinde amewataka wasichana kufanya vizuri na wayatumia mashindano ya
Airtel Rising Stars kufanikisha ndoto zao kupitia soka. Mechi ya
ufunguzi iliwakutanisha Chriss FC na Future Stars ambapo mechi
ilikwenda sare ya bila kufungana.
Katibu tawala Jiji la Arusha Ado Mapunda (RAS) akikagua timu katika
ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel
Rising Stars jijini Arusha jana.
Katibu tawala jiji la Arusha Ado Mapunda (RAS) akiongea na wachezaji
katika ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Airtel Rising Stars jijini Arusha jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...