Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akitoa mada katika  Kongamano la Vijana. Wakati wa kongamano hilo Balozi Mushy amewashauri vijana kufanya kazi na Taasisi za Umoja wa Mataifa ili kujipatia uzoefu wa kujielezea ikiwa ni pamoja na kujiamini. Kongamano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania Dkt. Natalia Kanem (Wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (wa kwanza kulia) wakimsikiliza Balozi Mushy (Hayupo pichani) wakati akiwasilisha Mada.
Juu na Chini ni picha ya Vijana waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza Balozi Mushy (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada.
Balozi Mushy akimwelezea jambo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi katika Kongamano la Vijana
Balozi Mushy (Katikati mwenye suti nyeusi) alipokuwa akiwasilisha mada ambapo pia alitaka kujua ni vijana wangapi wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2015, huku ikionekana idadi kubwa ya vijana waliohudhuria Kongamano hilo wamejiandikisha.
                                           Picha na Reginald Philip 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...