Mh.Mary Nagu –Waziri katika ofisi ya Raisi Mauhusiano na Uratibu na Mbunge wa Hanang akawaelimisha wananchi umuhimu wa kujiunga na CHF ILIYOBORESHWA katika siku ya uzinduzi .Kulia kwake ni Mkurugenzi wa shirika la PharmAccess kutoka Uholanzi Bw.Sicco Van Gelder ambao ndio wafadhili wa mradi huu wakishirikiana na NHIF.

Mgeni rasmi wa siku ya uzinduzi wa CHF ILIYOBORESHWA mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu Dr.Michael Kadeghe kukabidhi moja ya pikipiki tano zilizotolewa kwa maafisa wa CHF iliyoboreshwa ili kuwarahisishia kazi ya uandikishaji na uhamasishaji kwa wananchi wa tarafa tano za wilaya ya Mbulu.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akiwasha moja ya pikipiki tano alizokabidhi kwa maafisa wanaoshughulika na CHF ILIYOBORESHWA mbele ya umati wa wananchi wa wilaya ya Mbulu katika siku ya uzinduzi wa mradi huu kimkoa.
Anna Makange, Mbulu.
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Mh. Joel Bendera amezindua rasmi Mfuko wa Afya ya Jamii Uliboreshwa (iCHF) mkoani Manyara.Uzinduzi huo uliohudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mh.Mary Nagu (Mbunge - Hanang) na Waziri katika ofisi ya Raisi Mahusiano na Uratibu, Wakuu wa wilaya za Hanang na Mbulu pamoja Wawakilishi wa wizara ya afya na Ustawi wa Jamii, ulifanyika katika viwanja vya halmashauri ya mji wa Mbulu. Mkuu wa Mkoa alitoa maagizo kwa viongozi wa mkoa na wilaya kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri mradi huu na kuhamasisha wananchi wajiunge kwa wingi ili kufanikisha sera ya serikali ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...