Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania
Bi Devota Mdachi akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.
Adelhelm Meru (Mwenye miwani) kuzungumza na wafanyakazi alipotembelea bodi hiyo
jana.
Mmoja wa wafanyakazi wa TTB Bw. Geofrey Tengeneza
ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano akielezea jambo kwa Katibu Mkuu
alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania na kuzungumza na wafanyakazi. 
Baadhi ya wanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania
wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Dk
Meru alipokuwa akizungumza nao.
Na: Geofrey Tengeneza
Wizara
ya Maliasili na Utalii imeahidi kuupa kipaumbele mchakato wa kuifanya Bodi ya
Utalii Tanzania(TTB) kuwa Mamlaka ya Utalii Tanzania (TTA) kwa lengo la
kuiwezesha Bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kutekeleza majukumu yake
kikamilifu. Aidha Wizara hiyo imeitaka TTB kuangalia ni maeneo gani yanaweza kuwa ni
vyanzo vya mapato vitakavyoiwezesha Bodi kujiingizia fedha.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru
alipotembelea Makao makuu ya Bodi ya Utalii yaliyoko katika jengo la IPS
jijini Dar es salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bodi hiyo.
Dkt
Meru ameipongeza Bodi ya Utalii kwa kuendelea kufanya kazi
vizuri katika mazingira yenye changamoto nyingi hasa za kifedha zinazoikabili.
Amesema TTB ndiyo chombo chenye dhamana ya kutangaza vivutio vya utalii kwa
ujumla wake, hivyo kinapaswa kuwezeshwa kutimiza jukumu hilo kwa niaba ya nchi
badala ya kila taasisi kutangaza vivutio inavyosimamia.
“Tunawajibu
wa kuwawezesha TTB mtekeleze majukumu yenu vizuri kwa kuwa ninyi ndio hasa
mliokabidhiwa jukumu la kutangaza vivutio vyetu vyote vya utalii kama vile vya
kihistoria, fukwe, wanyama, milima na kadhalika” alisema.
Hii
ni ziara ya kwanza ya Dk Meru kutembelea Makao Makuu ya ofisi za Bodi tangu kuteuliwa
kwake kushika wadhifa huo. Bodi ya Utalii Tanzania ni moja ya taasisi zilizo
chini ya Wizara yake yenye jukumu la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania
ndani na nje ya nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...