
Taarifa iliyotolewa na Afisa ya
Habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imeeleza kuwa, viazi lishe hivyo ni aina
ya viazi vitamu vyenye asilimia 90 ya vitamini A vinavyohitajika katika mwili
wa binadamu ili kujenga ubongo wa watoto walio chini ya miaka 05, kuimarisha
afya ya wajawazito pamoja na uwezo wa kuona kwa kila mwanadamu. Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ni mingoni mwa Wilaya saba nchini, zilizochaguliwa na shirika
la kimataifa linaloshughulikia mazao ya viazi (CIP) kutekeleza mradi wa
uzalishaji wa viazi lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamini “A” ukilinganisha
na aina nyingine ya vyakula kama Mboga, Matunda na Mizizi.
Katika kutekeleza adhima hiyo, mradi
huo umeanza kutekekelezwa katika vikundi vya wakulima kwa kuotesha mbegu kwenye
maeneo yenye miundombinu ya umwagiliaji yaliyopo katika viijiji vya Igomaaa na Lugolofu pamoja bustani
zilizopo kwenye vijiji vya Lugema,
Mabaoni na Makungu.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa mbegu
zitakazozalishwa zitagawiwa kwenye vijiji 18 ambayo vimechaguliwa kutekeleza
mradi huo kwa kipindi cha miaka mitatu na utekelezaji mara babada ya kwa
kipindi cha mvua.
Aidha, endapo Viazi hivyo
vitazalishwa kwa wingi na kuongezwa thamani
vitaboresha kipato kwa mkulima kwani soko lake
linapatikana kwa urahisi huku vikiwa na uwezo wa kuzindikwa kwa utengenezaji wa
Kripsi, Mkate, Chapati, Biskuti, Juisi
na unga wa lishe. Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ni mingoni mwa Wilaya saba nchini, zilizochaguliwa na shirika
la kimataifa linaloshughulikia mazao ya viazi (CIP) kutekeleza mradi wa
uzalishaji wa viazi lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamini “A” ukilinganisha
na aina nyingine ya vyakula kama Mboga, Matunda na Mizizi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...