Katibu wa taswa mkoa wa Arusha Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la waandishi Agosti 29 uwanja wa kheikh Amri abeid mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha, Filex Ntibenda, kati kati mwenyekiti wa taswa mkoa Arusha, Jamila omar, Meneja matukio ya kampuni ya bia nchini TBL Chris Sarakana ambao wadhamini wakuu, na makamu mwenyekiti wa taswa Arusha, Andrea Ngobole
.
Mkuu wa
mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
tamasha la 10 la vyombo vya habari vya mkoa wa Arusha. ambalo
litafanyika Agosti 29 katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.
Akizungumza na waandishi wa habari Palace hoteli mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha, Jamila Omar na Katibu wa TASWA Arusha, Mussa Juma walisema maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwepo ujio wa timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.
Omar alisema Kauli mbiu ya Mwaka huu ya Tamasha hilo
ni kuwa,Uchaguzi bila vurugu inawezekana na timu zitachuana katika
michezo ya Soka, mbio zamagunia, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mpira
wa pete.Akizungumza na waandishi wa habari Palace hoteli mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha, Jamila Omar na Katibu wa TASWA Arusha, Mussa Juma walisema maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwepo ujio wa timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
tamasha hilo, Afisa matukio ya TBL Arusha, Chris Sarakana aliwataka
wanahabari na wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza na kuahidi TBL
itaendelea kushirikiana na wanahabari.
Awali
Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha,Mussa Juma alitaja timu nyingine
zitakazoshiriki ni TASWA Arusha, AJTC. Habari Maalum,Radio 5, Radio
,Faidika,Mj radio, Arusha one na ORS kutoka mkoa wa Manyara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...