Mtangazaji nguli wa kipindi cha BBC Idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim
Kikeke alipotembelea katika ofisi za MICHUZI MEDIA GROUP (MMG), leo jijini Dar es Salaam. Michuzi Blog ni blog pekee duniani ambayo BBC dira ya dunia imeichagua kushirikiana nayo katika kuendeleza libenke la habari ambapo kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kipindi maarufu cha habari cha Dira ya Dunia hurushwa na Globu ya Jamii. Pamoja na mambo mengi mengine Kikeke ameipongeza Michuzi Blog kwa kuendelea kuwa kinara wa habari za uhakika kwa Kiswahili zinazosomwa zaidi duniani, pia ameipongeza blog hiyo kwa kutimiza miaka 10 ya huduma za uhakika toka ilipoanza Septemba 8, 2005 jijini Helsinki Finland. Mahojiano na Salim Kikeke yatakujia karibuni ikiwa ni moja ya shamrashamra za kusherehekea miaka 10 ya Michuzi Blog. Stay tuned!
Mtangazaji nguli wa kipindi cha BBC Idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke akifanya mahojiano na mwandishi wa Michuzi tv online na Michuzi Blog, Chalila Kibuda, jijini Dar es Salaam leo.
Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Michuzi Media Group jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Michuzi Media Group, Muhidini Issa Michuzi, akiwa na Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...