Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

IMEELEZWA kuwa Mtoto chini ya mwezi hatakiwi kunywa maziwa yeyote isipokuwa ya mama yake, kutokana na maziwa ya ng’ombe  kuwa mazito na hayawezi kumsaidia mtoto katika kukua kwake.

Hayo ameyasema mtaalam wa lishe  wa Taasisi ya Chakula  lishe  nchini (TFNC),Neema Joshua wakati wa semina ya waandishi wa habari ya kuwajengea uwezo wa masuala ya Lishe,amesema maziwa ya ng’ombe yanatumika tu pale hakuna namna ya kuweza kupata maziwa mengine.

Amesema watoto chini ya miezi sita wanahitaji maziwa kwa mama na anatakiwa kupewa kila muda katika kuweza kumjenga mtoto kiakili.

Neema amesema katika suala la utapiamlo liko katika viwango vya juu ambapo mwaka 2010 ilikuwa na asilimia 42 hadi sasa imefikia asilimia 34.7 kwa takwimu za mwaka 2014.

Aidha amesema kuwa wale ambao wananyonyesha wakapata mimba akiwa ananyonyesha anaweza  kuuendelea kunyonyesha mtoto na bila kuathiri mimba nyingine.

Amesema wakati akinyonyesha huku ana mimba nyingine anatakiwa karibu na kujifungua miezi miwili aache kwa ajili ya kuupa mwili nguvu kwa mtoto atakayezaliwa na baada ya hapo anaendelea kunyonyesha wote wawili kwa kwanza akifikisha miwili ndipo anaweza kukoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tulipokuwa wanafunzi kule Mulago tulikuwa na professor wa paediatrics ambaye kiswahili chake kilikuwa matatizo sana. Nakumbuka akituambia kuwa, "Maziwa ya ngo'mbe ni kwa mtoto wa ngo'mbe"
    ibrahim

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...